IRAN-MAREKANI-TRUMP

Mwaka mmoja baada ya makubaliano kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran

Mwaka baada ya kutekelezwa kwake, makubaliano ya kihistoria kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran yamedhoofika na kuwasili kwa Donald Trump katika Ikulu ya White House. Rais mteule wa Marekani anapinga vikali nakala hii inayochukuliwa kama moja ya mafanikio makubwa ya Rais wa Iran Hassan Rouhani.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Hassan Rohani, mwaka 2015 katika chumba cha udhibiti wa kituo cha nyuklia cha Bushehr.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Hassan Rohani, mwaka 2015 katika chumba cha udhibiti wa kituo cha nyuklia cha Bushehr. MOHAMMAD BERNO / IRANIAN PRESIDENCY / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mwaka mmoja baada ya kutekelezwa kwa mpango wa nyuklia wa Iran na kuondolewa kwa baadhi ya vikwazo vya kimataifa, Rais Hassan Rouhani anaridhishwa na mafanikio ya mauzo ya mafuta.

Iran pia imefanikiwa katika kuvutia makampuni makubwa ya kimataifa kama vile Total, kampuni ya Ufaransa na Shell inayomilikiwa na Uingereza na Uholanzi kwa kuendeleza sekta yake ya mafuta na gesi . Vile vile, Tehran ilisaini mikataba miwili mikubwa ya ununuzi wa ndege 100 aina ya Airbus na Boeing 80 na kusitisha miaka zaidi ya 37 ya vikwazo vya Marekani.

Hata hivyo, hali haijabadilika. Mfumuko wa bei umepungua hadi chini ya 10%, lakini ukosefu wa ajira umeongezeka na kufikia 12.7% kwa watu wenye nguvu za kufanya kazi.

Swala la kuingia madarakani kwa Donald Trump nchini Marekani limetishia mpango wa nyuklia. Rais mteule wa Marekani aliyataja makubaliano ya mpango wa nyuklia wa Iran kama ya "kutisha". Watu alioteua katika serikali yake wanajulikana kwamisimamo yao dhidi ya Tehran. Vile vile, Bunge la Congress la Marekani, lenye wawakilishi wengi kutoka chama cha Republican, linaandaa vikwazo vipya dhidi ya Tehran.

Kwa masharti haya, Rais Rohani ambaye atawania kwa muhula wa pili katika uchaguzi wa urais wa mwezi Mei ana kazi ngumu.