UKRAINE-URUSI-USALAMA

Vurugu zaongezeka Ukraine: Moscow na Kiev walaumiana

Gari ya kijeshi karibu na mji wa Avdiyivka nchini Ukraine Februari 1, 2017.
Gari ya kijeshi karibu na mji wa Avdiyivka nchini Ukraine Februari 1, 2017. REUTERS/Gleb Garanich

Kwa uchache watu sita waliuawa kwenye uwanja wa vita mashariki mwa Ukraine, siku ya nne ya mapigano baina ya vikosi vya Ukraine na waasi wanaoungwa mkono na Urusi. Watu Ishirini, ikiwa ni pamoja na raia wa kawaidi pamoja na wapiganaji, wameuawa tangu Jumapili Januari 29.

Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Ulaya unalaani uvunjwaji wa mktaba wa usitishwaji wa mapigano kati ya pande hizo mbili. Moscow na Kiev wameanza kulaumiana.

Moscow imefutilia mbali dhidi ripoti ya waangalizi wa OSCE wanawashutumu viongozi wa eneo lililojitenga na Ukraine la Donbass na Urusi kwa kuchochea machafuko katika eneo hilo la Donbass. "Tunachokiona ni uchokozi wa majeshi ya Ukreni na wanamgambo wake," msemaji wa Ikulu ya Kremlin ameviambia vyombo vya habari.

Dmitry Peskov anayachukulia maneno ya Naibu Waziri wa Ulinzi wa Ukreni kama ushahidi kwamba serikali ya Kiev imeamua kuendesha mashambulizi. Igor Pavlosvsky alisikika akisema, "mita kwa mita, hatua kwa hatua, vijana wetu wamesonga mbele. "Kwa mujibu wa Yuri Ushakov, mshauri wa Rais wa Urusi, serikali ya Kiev inataka kuujaribu utawala mpya wa Marekani, kuona kama uko tayari kusaidia katika makosa ya majeshi ya Ukreni. Na Ukraine inataka kuchukua kisingizio cha mapigano mapya ili kujitoa katika mikataba ya Minsk, ameongeza Igor Pavlosvsky.

Pia, Kremlin imebaini kwamba hali nchini Ukraine ni sababu nyingine ya kuanzisha tena upya mazungumzo na ushirikiano kati ya Urusi na Marekani. Swala hilo lilizungumzwa na Vladimir Putin pamoja na Donald Trump wakati wa mkutano wao Jumamosi iliyopita, lakini marais hao wawili hawakujadi undani wa swala hilo.