Urusi yapinga kuirejeshea Ukraine sehemu yake ya Crimea

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergueï Lavrov wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Moscow, Januari 17, 2017.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergueï Lavrov wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Moscow, Januari 17, 2017. REUTERS/Sergei Karpukhin

Urusi imekataa katu katu kuirejeshea Ukraine shemu yake ya zamani ya Crimea, Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imetangaza Jumato wiki hii, ikiwa ni jibu kwa kauli iliyotolewa siku moja iliyopita na msemaji wa Donald Trump.

Matangazo ya kibiashara

"Kamwe hatutorejesha moja ya sehemu zetu. Crimea ni sehemu ya ardhi ya Urusi," Maria Zakharova, msemaji wa wizara, amesema katika mkutano na waandishi.

Sean Spicer, msemaji wa Ikulu ya White House, alisema Jumanne kuwa rais wa Marekani anatarajia kuwa Urusi imo mbioni kurejesha eneo la Crimea ilililopokonya mwezi Machi 2014 kwa Ukraine. "Wakati huo huo, anasubiri kuwepo kwa maelewano mazuri na Urusi, "Sean Spicer ameongeza.

Maria Zakharova pia ametangaza kwamba kutakuepo na mazungumzo kati ya Waziri wa mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov na mwenzake wa Marekani, Rex Tillerson, ambao yatafanyika wakati wa mkutano wa Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni kutoka mataifa ya G20 ambao umepangwa kufanyika Alhamisi na Ijumaa katika mji wa Bonn, nchini Ujerumani.