KOREA KASKAZINI-MALAYSIA-USHIRIKIANO

Korea Kaskazini yaomba mwili wa Kim Jong-nam kurejeshwa nchini

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, ndugu wa kambo wa Kim Jong-nam aliyeuawa nchini Malaysia.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, ndugu wa kambo wa Kim Jong-nam aliyeuawa nchini Malaysia. KCNA/via Reuters

Korea Kaskaziini imeitaka Malaysia, kusafirisha mwili wa ndugu wa karibu wa kiongozi wake Kim Jong-un aliyeuawa wiki hii nchini humo. Ripoti zinasema kuwa, Kim Jong-nam alipewa sumu wakati alipokuwa anajiadaa kupanda ndege katika uwanja wa l Kuala Lumpur.

Matangazo ya kibiashara

Mamlaka nchini Malaysia inamshikilia mwanamke mmoja kutoka Burma kama sehemu ya uchunguzi wa mazingira ya kifo cha ndugu wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, liliarifu Jumatano shirika la habari la Malaysia la Bernama.

Mwanamke huyo alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur unaotumiwa na mashirika ya ndege ya gharama nafuu, shirika hilo lilisema likimnukuu afisa mwandamizi wa polisi.

Hakuna maelezo zaidi ambayo yalitolewa kwa sasa na polisi ya Malaysia haijazungumza lolote mpaka sasa.

Hata hivyo, ripoti zinasema kuwa serikali ya Malaysia inasisitiza kuwa haitakubali shinikizo zozote kutoka Korea Kaskazini, wakati huu mwanamke mmoja akishikiliwa kwa madai ya kuhusika na kifo hicho.

Korea ya Kusini inawashuku wanawake wawili ambao ni maafisa wa Idara ya ujasusi ya Korea Kaskazini kuwa ndio walimpa sumu Kim Jong-nam, ndugu wa kambo wa Kim Jong-un Jumanne katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur, kwa amri ya kiongozi wa Korea Kaskazini.

Kim Jong-nam, ambaye alikuwa akiondoka katika mji wa Macau, alijisika vibaya kiafya katika uwanja huo wa ndege na kifo chake kilitokea wakati aliposafirishwa hospitalini, polisi ya Malaysia imesema.