Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-MALAYSIA-USHIRIKIANO

Mauaji ya Kim Jong-nam: mtuhumiwa wa tatu akamatwa

Picha iliyonaswa na televisheni ya China inaonyesha moja ya watuhumiwa (kavaa njano kichwani) akipelekwa na Polisi ya Malaysia.
Picha iliyonaswa na televisheni ya China inaonyesha moja ya watuhumiwa (kavaa njano kichwani) akipelekwa na Polisi ya Malaysia. REUTERS
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Mtu wa tatu amliyekamatwa ni rafiki wa mwanamke wa pili aliyekamatwa. Wakati ambapo mtuhumiwa wa kwanza alikuwa na pasipoti ya Vietnam, mtuhumiwa wa pili alikua na vyeti vya Indonesia.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Idara ya Ujasusi ya Korea Kusini, Kim Jung-nam alikuwa alilengwa na jaribio la mauaji mwaka 2012. Lakini kwa miaka mingi alikua akiishi na familia yake katik mji wa Macao.

Kwa mujibu wa gazeti la South China Morning Post, gazeti la Kiingereza la Hong Kong, ndugu wa kambo wa kiongozi wa sasa wa Korea Kaskazini, alikua anajua kuwa maisha yake yako hatarini. "Alijua kwamba ndugu yake alikua na lengo la kumua na kwamba siku zake zinahesabiwa," alisema mmoja wa marafiki zake ambao alishangaa kutokuwa na habari ya Kim Jong-nam, ambaye alikua akiitwa na marafiki zake wa mji wa Macao kwa jina la "John".

Hofu ya mtoto wa Kim Jong-Il, mjukuu wa Kim Il-sung ya kuuawa na na ndugu yake mdogo wa kambo ilizidi baada ya kuuawa kwa mjomba wao mwaka 2013, kwa sababu mjomba wao huyo ndiye aliyemlea na kumlinda baada ya kifo cha baba yake KimJong-Il.

Wakati huo huo polisi nchini Malaysia wamefanikiwa kuwakamata washukiwa wengine wawili wanaohusishwa na kifo cha Kim Jong-nam.

Waliokamatwa ni mwanamke na mwanamume wanaoaminiwa kuwa ni wapenzi, na wanaendelea kuchunguzwa baada ya kuwepo kwa ripoti kuwa Kim Jong-nam alipewa sumu.

Pyongyang imesema inataka mwili huo lakini, Malaysia imesema haitashinikizwa na yeyote.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.