Pata taarifa kuu
MALAYSIA-KOREA KASKAZINI-USHIRIKIANO

Malaysia yakataa katu katu kusafirisha mwili wa Kim Jong-nam

mpur le 13 février 2017. Il avait 45 ans.
mpur le 13 février 2017. Il avait 45 ans. Joongang Ilbo/News1 via REUTERS
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Serikali ya Malaysia imesema kuwa haitaruhusu kusafirishwa kwa mwili wa Kim Jong-nam, ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini aliyeuawa mwishoni mwa juma, hadi pale itakapopewa sampuli ya vinasaba, maarufu kama DNA, kutoka kwa familia yake licha ya maombi kutoka utawala wa Pyongyang.

Matangazo ya kibiashara

Wapelelezi nchini humo wanajaribu kupata ukweli wa kiini cha mauaji yake, ambayo utawala wa Korea Kusini unadai kuwa yalitekelezwa kwa kutumia sumu iliyokuwa imebebwa na wanawake wawili wanaofanya kazi na utawala Korea Kaskazini.

Wachunguzi wa vinasaba hii leo wameendelea kukagua mwili wa Jong-Nam kujaribu kutambua aina ya sumu iliyotumiwa kumuua kwa kupuliziwa usoni wakati alipojaribu kupanda ndege mwanzoni mwa wiki hii.

Utawala wa Korea Kaskazini ulikataa wazo la mwili wa Kim Jong-nam kufanyiwa uchunguzi, lakini utawala wa Kuala Lumpur ulisimama kidete na kusisitiza kufanyia uchunguzi mwili wake.

Hadi sasa hakuna mwanandugu yeyote aliyejitokeza kuutaka mwili wake na utawala wa Kuala Lumpur unasisitiza kwanza upewe Sampuli za DNA kutoka kwa mmoja wa wanafamilia.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.