Mauaji ya Kim: Malaysia yamuita nyumbani balozi wake Korea Kaskazini
Serikali ya Malaysia imechukua uamuzi wa kumuita balozi wake nchini Korea Kaskazini kufuatia mvutano unaoendelea kati ya Malaysia na Korea Kaskazini kutokana na kifo cha Kim Jong-nam, ndugu wa kambo wa kiongozi wa sasa wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.
Imechapishwa:
Kifo cha Kim Jong-un kilichotokea wiki iliyopita kwenye uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur, nchini Malaysia. Kwa mujibu wa maafisa wa usalama wa Malaysia wanashuku kwamba huenda Kim Jong-un aliuawa kwa sumu.
Watu kadhaa wamekamatwa kwa jali ya uchunguzi.
Wiki iliyopita Korea Kaskazini ilitaka mwili wa Kim Jong-un urejeshwe nyumbani, lakini serikali ya Malaysia ilifutilia mbali hoja hiyo na kutaka uchunguzi ufanyike ili wahusika wajulikane na shria ifuate mkondo wake.
Hata hivyo serikali ya Malaysia imesisitiza kuwa itaendelea na uchunguzi na kwamba ina mamlaka ya kufanya uchunguzi huo kwa sababu Kim Jon-un alifia katika ardhi yake.