Malaysia yampa balozi wa Korea Kaskazini saa 48 kuondoka nchini humo
Imechapishwa:
Malaysia imemfukuza balozi wa Korea Kaskazini na kumpa saa 48 kuondoka nchini humo, hatua ambayo ni mpasuko mkubwa katika uhusiano wa kibalozi baina ya nchi hizo, kufuatia mauaji ya ndugu wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Nam katika uwanja wa ndege mjini Kuala Lumpur mwezi uliopita.
Kim Jong-Nam, aliyekuwa na umri wa miaka 45, aliuawa kwa sumu aina ya VX Februari 13 , sumu inayoharibu neva.
Korea Kaskazini haijakubali utambulisho wa mtu aliyeuawa lakini imerejea kuhujumu uchunguzi wa mauaji, ikiishutumu Malaysia kwa kushirikiana na maadui zake.
Tayar wanawake wawili wameshitakiwa nchini Malaysia kwa kuhusika na mauaji ya Kim Jong Nam