KOREA KASKAZINI-MALAYSIA

Korea Kaskazini yawazuia raia wa Malaysia, Kuala Lumpur nayo yajibu mapigo

Nchi ya Korea Kaskazini imetangaza kuwazuia kuondoka nchini humo raia wa Malaysia, hatua inayoonekana ni kama ulipizaji kisasi kwa utawala wa Kuala Lumpur ambao ulimfurusha nchini mwake balozi wa Korea Kaskazini katika mvutano kuhusu kifo cha Kim Jong-Nam, kaka wa Kim Jong-Un.

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un ambaye ametangaza kuzuia kuondoka nchini mwake kwa raia wa Malaysia
Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un ambaye ametangaza kuzuia kuondoka nchini mwake kwa raia wa Malaysia KCNA/via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu wa kushangaza wa Serikali ya Pyongyang, ambao umeelezwa na waziri mkuu wa Malaysia unamaanisha kuwaweka raia wake mateka, umekuja wakati huu Korea Kaskazini ikikabiliwa na shinikizo kubwa toka kwa jumuiya ya kimataifa kutokana na jaribio lake la kombora la masafa marefu mwishoni mwa juma.

Hatua hii imekuja wakatyi ambapo sintofahamu ya kidiplomasia baona ya nchi hizo mbili imezidi kuonekana dhahiri baada ya mauaji ya uwanja wa ndege ya kaka wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Nam, aliyeuawa kwa kutumia sumu.

Tangazo la Serikali ya Korea Kaskazini lililotolewa kupitia televisheni ya taifa,limesema kuwa uamuzi wa Serikali ni wa muda.

Zuio hili litaendelea kuwepo hadi pale usalama wa raia wake walioko Malaysia utakapohakikishwa na Serikali ya Kuala Lumpur na namna bora ya kushughulikia kesi ya ndugu yao aliyeuawa.

Taarifa zinasema kuwa zaidi ya raia 11 wa Malaysia wanaelezwa kuwepo Korea Kaskazini.

Waziri mkuu Najib amekashifu hatua hii ya Korea Kaskazini ambapo katika kuonesha kujibu mapigo, ametangaza kuzuia harakati zozote za raia wa Korea Kaskazini walioko nchini humo, raia wanaokadiriwa kufikia zaidi ya 1000.

Wizara ya mambo ya ndani, awali ilitangaza kuwa makataa haya yangewahusu maofisa wa ubalozi peke yake,