HONG KONG-CHINA

Kiongozi mpya Carrie Lam kuiunganisha Hong Kong

Kiongozi mpya wa Hong Kong Carrie Lam
Kiongozi mpya wa Hong Kong Carrie Lam REUTERS/Vincent Yu/POOL

Kiongozi mpya wa Hong Kong Carrie Lam ameahidi leo jumapili kurekebisha mipasuko ya kisiasa baada ya kushinda uchaguzi uliopingwa na wanaharakati wa demokrasia ambao wanahofu ya kupoteza uhuru wa eneo hilo.

Matangazo ya kibiashara

Hong Kong ilijitenga tangu ilipokabidhiwa mikononi mwa China baada ya kutawaliwa na wakoloni waingereza mwaka 1997.

Hata hivyo miaka 20 baadae kumekuwa na wasiwasi kuwa Beijing haitambui mkataba wa makabidhiano uliobuniwa kulinda uhuru wa Hong Kong.

Mtumishi wa zamani wa umma aliyechaguliwa kuwa kiongozi mkuu na kamati inayounga mkono China alionekana kuwa chaguo la Beijing kuongoza.

Wakosoaji wanasema atazidisha mgawanyiko katika mji huo licha ya Lam kuahidi kuiunganisha  Hong Kong.