URUSI

Marekani na EU zalaani kukamatwa kwa kiongozi wa upinzani nchini Urusi

Polisi walivyomkamata  Alexei Navalny kiongozi Mkuu wa upinzani nchini Urusi Machi 26 2017 wakati wa maandamano jijini Moscow
Polisi walivyomkamata Alexei Navalny kiongozi Mkuu wa upinzani nchini Urusi Machi 26 2017 wakati wa maandamano jijini Moscow REUTERS/Maxim Shemetov

Kiongozi Mkuu wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny, amekamatwa baada ya kutokea kwa maandamano makubwa ya kutaka kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Dmitry Medvedev mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Moscow.

Matangazo ya kibiashara

Maelfu ya wanaandamanaji walijitokeza kuandamana wakidai kujiuzulu kwa Waziri Mkuu huyo kwa madai ya ufisadi katika serikali yake.

Maandamano hayo yalizua makabiliano makali katika miji mbalimbali nchini humo kati ya waandamanaji na maafisa wa usalama.

Navalny anayepanga kuwania urais mwaka 2018, ni miongoni mwa waandamanaji 5000 waliokamatwa na wanazuiwa katika miji mbalimbali.

Marekani imelaani kukamatwa kwa kiongozi huyo wa upinzani na waandamanaji wengine.

Muungano wa Umoja wa Ulaya nao umelaani hatua hiyo na kutaka waandamanaji hao kuwaachilia huru wafungwa hao.

Serikali ya Urusi imekuwa ikilaaniwa nje ya ndani ya nje hiyo hasa nchi za Magharibi kwa kuminya wanasiasa wa upinzani nchini humo.