KOREA KUSINI

Korea Kusini: Waendesha mashtaka wataka kutolewa hati ya kukamatwa kwa Park Geun-Hye

Rais wa zamani wa Korea Kusini  Park Geun-hye  akiwasili kuhojiwa katika Ofisi za kiongozi wa Mashtaka ya umma Machi 21 2017
Rais wa zamani wa Korea Kusini Park Geun-hye akiwasili kuhojiwa katika Ofisi za kiongozi wa Mashtaka ya umma Machi 21 2017 REUTERS/Kim Hong-Ji

Viongozi wa Mashtaka nchini Korea Kusini wanasema wataomba kukamatwa kwa rais wa zamani wa nchi hiyo Park Geun-Hye.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hi inakuja baada ya Bi.Park kuhojiwa kwa madai ya ufisadi na utumizi mbaya wa madaraka tangu alipokuwa rais mwaka 2012.

Rais huyo wa zamani ambaye tayari ameondolewa madarakani na bunge, anatuhumiwa pia kwa kuhusika na utoaji rushwa na kutoa siri za serikali.

Hata hivyo, kiongozi huyo wa zamani amekuwa akikanusha madai dhidi yake na kuyataja kuwa ya kisiasa .

Licha ya madai hayo, tayari mshirika wa karibu wa rais Park, Choi Soon-Sil amefunguliwa mashtaka kwa kulazimisha shirika moja nchini humo kutoa malipo ya Dola Milioni 70 yaliyomnufaisha kiongozi huyo wa zamani.