Mtu mmoja apatikana amekufa ndani ya tumbo la Chatu Indonesia
Imechapishwa:
Raia mmoja wa Indonesia aliyekuwa akitafutwa na familia yake baada ya kupotea, amepatikana amekufa ndani ya tumbo la chatu, polisi nchini humo wamethibitisha.
Raia huyo Akbar alipotea siku ya Jumapili kwenye kisiwa cha Sulawesi, baada ya kuwa amameliza kuvuna mafuta ya nazi.
Wakati wakimtafuta raia huyo, polisi nchini humo waliambia shirika la habari la Uingereza kuwa, walimpata mtu huyo akiwa tumboni mwa nyoka huyo.
Chatu huyo mwenye urefu wa mita 7, alilazimika kupasuliwa na mwili wa raia huyo kukutwa ndani yake.
Nyoka huyu ni miongoni mwa nyoka wanaotajwa kuwa warefu zaidi duniani na wamekuwa wakiwabana pumzi mawindo yao kabla ya kuwameza wazima wazima.
Ni mara chache sana kuona Chatu wakimeza mtu au kuua licha ya kuwa kumekuwa na taarifa kuwa mara nyingi wamekuwa wakimeza watoto wadogo.
Polisi kwenye kisiwa hicho wanasema walipokea taarifa kutoka kwa wanakijiji kuwa Akbar alikuwa amepotea katika muda wa saa 24.
“Hawakumpata Akbar baada ya kumtafuta, lakini wanakijiji walimuona chatu ambaye alikuwa hawezi kutembea kwenye bonde moja, wakawa na wasi wasi kuwa huenda alikuwa amemmeza Akbara, walipompasua Akbar alikuwa ndani yake.
Wataalamu wa masuala ya nyoka wanasema kuwa nyoka wa aina hii mara nyingi anauwezo na huwa anatafuta mawindo ambayo ni makubwa kama vile mbwa na kwamba huwa wanawakwepa sana binadamu na kwamba huwa wanakaa kwenye minazi wakiamini ndio mawindo mazuri.