CHINA-KOREA KASKAZINI-USALAMA

China: Tuna hofu na vitisho vya nyuklia vya Korea Kaskazini

Korea Kaskazini ilionyesha uwezo wake wa kivita wakati wa gwaride la Aprili 15, 2017 mjini Pyongyang.
Korea Kaskazini ilionyesha uwezo wake wa kivita wakati wa gwaride la Aprili 15, 2017 mjini Pyongyang. REUTERS/Damir Sagolj

Siku nne baada ya Korea ya Kaskazini kutangaza kwamba itakua ikifanya majaribio yake ya nyuklia kila wiki au kila mwezi, China imesema kuwa ina waswasi kuhusu mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China, Lu Kang, amebaini kwamba nchi yake imepinga vitendo au matamshi ambayo huenda yakasababisha hali zaidi ya wasiwasi nchini mwake.

''China ina wasiwasi mkubwa kuhusu mpango wa nuklia wa Korea Kaskazini na utengenezaji wa silaha, '' Lu Kang amesema.

Naibu wa waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini akiwa mjini Pyongyang amesem akuwa nchi yake itaendelea kuyafanyia majaribio ya makombora yake na itarusha bomu la nuklia iwapo kwamba Marekani itataka kuishambulia.

Mapema wiki hii Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence ambaye alikua alizuru China alionya Korea Kaskazini kutoijaribu Marekani, akibaini kwamba wakati wa subira dhidi ya Pyongyang umekwisha.