Meli za Japan zawasili katika rasi ya Korea Kaskazini

USS Carl Vinson-Ping ikielekea katika Bahari ya Japani, na hivi karibuni kundi la meli za Japan zinaikaribia.
USS Carl Vinson-Ping ikielekea katika Bahari ya Japani, na hivi karibuni kundi la meli za Japan zinaikaribia. AFP/US Navy/MC2 Sean M. Castellano

Saa chache baada ya Korea Kaskazini kutangaza kuwa iko tayari kuzamisha meli ya kubeba ndege ya Marekani inayoelekea rasi ya Korea, kwa mjibu wa vyombo vya habari vya Korea Kaskazini, tayari kundi la meli za Japan zimewasili katika rasi ya Korea Kaskazini.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo inasadikiwa kuwa kundi la meli za Marekani zikiongozwa na Vinson zinatarajiwa kuwasili katika rasi ya Korea wiki hii.

Meli hizo zilitumwa na Rais Donald Trump baada ya onyo kuhusu uvumilivu kumalizika dhidi ya mpamgo ya nuklia ya Korea Kasakazini.

Taarifa katika gazeti la Rodong Sinmun lilisema kuwa meli ya Marekani ya USS Carl Vinson itazamishwa kwa shambulizi moja.

Gazeti la Rodong Sinmum limesema "vikosi vyetu viko tayari kuzamisha meli hiyo ya kubeba ndege ya Marekani kwa shambulizi moja tu.

Vita vya maneno viliibuka baada tu ya Marekani kuionya Korea Kaskazini kutoendelea kufanya majaribio ya makombora ya masafa marefu pamoja na kuendeleza mpango wake wa nyuklia.

Hivi karibuni Korea Kaskazini iliapa kuendelea na mpango wake pamoja na majaribio ya makombora kila wiki na kila mwezi kwa minajili ya usalam wake.