MAREKANI-KOREA KASKAZINI-USALAMA

Trump : Korea Kaskazini ni tisho la ulimwengu

Donald Trump aendelea kuinyooshea kidole cha lawama Korea Kaskazini.
Donald Trump aendelea kuinyooshea kidole cha lawama Korea Kaskazini. REUTERS/Kevin Lamarque

Saa chache baada ya nyambizi ya jeshi la Marekani kuwawasili katika pwani ya Korea Kusini, Korea Kaskazini imefanya zoezi kubwa la kijeshi ambapo ufyatuaji wa risasi ulifanyika ili kuadhimisha miaka 85 tangu uzinduzi wa jeshi lake.

Matangazo ya kibiashara

Wasiwasi umeendelea kuongezeka kuhusu uwezekano wa Korea Kaskazini kufanya jaribio jingine la kombora au silaha za nyuklia.

Mamlaka ya Korea Kusini imesema kuwa idadi kubwa ya vifaa vyake vya kijeshi vimepelekwa katika eneo la Wonsan kwa zoezi la kijeshi.

Korea Kusini pia imesema kuwa wanamaji wake wamekuwa wakifanya mazoezi ya pamoja na meli za kijeshi za Marekani.

Mapema mjini Washington rais Trump alisema kuwa Korea Kaskazini ni tisho la ulimwengu.

Hayo yakijiri, katika tukio ambalo si la kawaida, bunge lote la Seneti nchini Marekani limealikwa kwa kikao cha kupashwa habari kuhusu Korea Kaskazini siku ya Jumatano katika ikulu ya White House.

Nyambizi ya USS Michigan hutumia nguvu za nyuklia na hubeba makombora aina ya 154 Tomahawk na wanajeshi 60 pamoja na meli nyambizi nyingine ndogo, gazeti la Korea Kusini la Chosun Ilbo limeripoti.

Meli hiyo inatarajiwa kushiriki kwenye mazoezi ya kijeshi pamoja na kundi la meli zinazoongozwa na Carl Vinson, kundi ambalo lilitumwa eneo la Korea kuonyesha ubabe wa kijeshi wa Marekani.

Des soldats nord-coréens lors de la célébration mardi à Pyongyang du  85e anniversaire de la création de leur armée.
Des soldats nord-coréens lors de la célébration mardi à Pyongyang du 85e anniversaire de la création de leur armée. Mandatory credit Kyodo/via REUTERS