MAREKANI-KOREA KASKAZINI-USALAMA

Korea Kaskazini kukabiliwa na vikwazo vikali vya Marekani

Donald Trump aendelea kuionya Korea Kaskazini.
Donald Trump aendelea kuionya Korea Kaskazini. REUTERS/Kevin Lamarque

Marekani inatarajiwa kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini, katika jitihada za kuifanya nchi hiyo kuachana na majaribio yake ya silaha za Nyuklia.

Matangazo ya kibiashara

Mpango huu wa rais Donald Trump, umetanagzwa wakati wa mkutano wa Maseneta 100.

Mamlaka ya rais Donald Trump imewaelezea maseneta wote 100 wa bunge la taifa hilo kuhusu tishio la Korea Kaskazini na kubaini mikakati ya kuishinikiza Pyongyang kupitia vikwazo vya kiuchumi na vile vya kidiplomasia.

Lengo ni kuilazimu Korea Kaskazini kusitisha mpango wa makombora ya masafa marefu pampja na ule wa Kinyuklia.

Hali ya wasiwasi imeendelea kushuhudiwa katika eneo la Korea, lakini pia kati ya Marekani na Korea Kaskazini ambazo zimeendelea kutishiana kuwa zitashambuliana.