MAREKANI-KOREA KASKAZINI-USALAMA

Trump aionya kwa mara nyingine Korea Kaskazini

Donald Trump anasema hatokubaliana na mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.
Donald Trump anasema hatokubaliana na mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini. REUTERS/Kevin Lamarque

Rais wa Marekani Donald Trump, kwa mara nyengine tena, ameonya kwamba mzozo mkubwa utazuka na Korea Kaskazini kuhusu mpango wake wa nyuklia na ule wa kutengeza makombora ya masafa marefu.

Matangazo ya kibiashara

Awali Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson alisema China imeionya Korea Kaskazini kutarajia vikwazo iwapo itathubutu kufanya majaribio mengine ya kinyuklia.

Rais Donald Trump alimpongeza mwenzake wa China Xi Jinping akisema amekuwa akijaribu kwa kila njia kuishinikiza Korea Kaskazini kuachana na mpango wake wa nyuklia na kutengeneza makombora ya masafa marefu.

Katika mahojiano na chombo cha habari cha Reuters Bw Trtrump amesema kuwa angependelea mzozo huo kukabiliwa kidiplomasia lakini amesema hiyo itakuwa vigumu kuafikia.

Wakati huo huo Korea Kaskazini imetoa kanda ya video ya propaganda ikionyesha itakavyoishambulia Marekani.

Kanda hiyo inashirikisha Ikulu ya Whitehouse na ndege ya kubeba ndege za kijeshi inayokabiliwa na inakamilika na Ikulu hiyo ikilipuka.

Hayo yakijiri wizara ya Ulinzi nchini Marekani imesema kuwa inamchunguza aliyekuwa mshauri wa maswala ya usalama wa rais Donald Trump kuhusu malipo aliyopokea kutoka kwa kampuni zinazohusishwa na serikali ya Urusi.

Wachunguzi wa bunge la Congress wanasema kuwa wakati jenerali Flynn alipoondoka katika jeshi alionywa kutochukua malipo yoyote ya serikali ya kigeni bila ruhusa.

Michael Flynn alijiuzulu katika serikali ya Trump baada ya siku 24 pekee kuteuliwa kwenye nafasi hiyo baada ya kubainika kwamba alimdanganya makamu wa rais kuhusu mawasiliano yake na balozi wa Urusi.