MAREKANI-JAPAN-KOREA KASKAZINI-USALAMA

Meli ya Japan yaongozana na meli ya Marekani kwenye bahari ya Japan

Meli kubwa ya kivita ya Marekani USS Carl Vinson.
Meli kubwa ya kivita ya Marekani USS Carl Vinson. REUTERS

Japan imetuma meli yake kubwa ya kubeba helikopta ambayo imepewa jina la Izumo, kuifuata meli ya kubeba mizigo na vifaa vya kijeshi ya Marekani ambayo inapitia katika maeneo ya bahari ya Japan.

Matangazo ya kibiashara

Shirika la habari la Kyodo limesema meli hiyo imeondoka kwenye kambi yake eneo la Yokosuka kusini mwa Tokyo kwenda kuungana na meli hiyo ya kusafirisha bidhaa za jeshi la Marekani, na kwamba itaisindikiza hadi kwenye pwani ya Shikoku magharibi mwa Japan.

Meli ya Marekani inaelekea kufikisha mafuta kwa meli nyingine za chi hiyo zinalohudumu eneo hilo, ikiwemo meli yake kubwa ya kubeba ndege ya Carl Vinson na meli zinazoandamana na meli hiyo karibu na rasi ya Korea.

Hivi karibuni Korea Kaskazini imetishia kuizamisha Carl Vinson pamoja na nyambizi ya Marekani, huku wasiwasi ukiendelea kuongezeka eneo hilo.

Itafahamika kwamba Kora Kaskazini ilifanya jaribio la kurusha kombora ambalo lilifeli Jumapili, licha ya vitidho vya Marekani na Umoja wa Mataifa kutokana na mpango wake wa kutengeneza silaha za nyuklia na kufanya majaribio ya makombora ya masafa marefu.

Vita vya maneno vimeendelea kushuhudiwa kati ya mataifa hayo mawili, huku majirani wa Korea Kaskazini wakiendelea kuwa na wasiwasi.