MAREKANI-KOREA KASKAZINI-USALAMA

Majeshi ya Marekani na Korea Kusini wafanya mazoezi ya kijeshi

Ndege ya kivita ya Marekani B-1B  juu ya anga ya kambi ya Pyeongtaek, Korea Kusini, Septemba 13, 2016.
Ndege ya kivita ya Marekani B-1B juu ya anga ya kambi ya Pyeongtaek, Korea Kusini, Septemba 13, 2016. REUTERS/Kim Hong-Ji/File photo

Korea Kaskazini imeshtumu Marekani kuitumia rasi ya Korea katika mawazo ya vita ya nyuklia. Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un hakufurahia uwepo wa ndege za kivita wakati wa mazoezi ya pamoja kati ya majeshi la Marekani na Korea Kusini.

Matangazo ya kibiashara

Mvutano unaendelea kuongezeka katika eneo hilo ambapo Korea Kaskazini imehadi kufanya katika siku zijazo jaribio la sita la nyuklia.

Korea Kaskazini inasema ndege mbili za kivita za Marekani zimefanya mazoezi ya kurusha mabomu ya kinyuklia dhidi ya maeneo muhimu ya Korea Kaskazini na kuushtumu utawala wa Trump kutaka kuendesha mashambulizi.

Hali bado ni tete katika eneo hilo kwa wakati huu, wakati ambapo Marekani na Korea Kusini zikifanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi. Lakini wakati huu hali ni tofauti ile ya awali: Pyongyang imeongezea kasi mpango wake wa kijeshi uliopigwa marufuku na Umoja wa Mataifa, kwa kufanya katika wiki za karibuni majaribio matatu ya makombora na kuahidi jaribio jingine la nyuklia katika siku zijazo.

Ndege za kuangusha mabomu za Marekani zapaa Korea

Maafisa wa Korea Kusini wamesema ndege mbili za Marekani za kuangusha mabomu zimepaa juu ya anga la rasi ya Korea.

Ndege hizo za kivita zilipaa angani kama sehemu ya juhudi za kuzuia vitisho na uchokozi kutoka kwa Korea Kaskazini.

Ndege hizo aina ya B1-B zilishiriki operesheni ya pamoja na ndege za kivita za Korea Kusini.

Kupaa kwa ndege hizo kumetokea wakati ambapo Rais Trump ametoa taarifa za kukanganya kuhusu msimamo na sera ya Marekani dhidi ya Pyongyang.

Bw Trump aliambia Fox News kwamba msimamo wa Korea Kaskazini kuhusu mpango wake wa kufanyia majaribio makombora ya nyuklia ni wa kukera.