KOREA KASKAZINI

Korea Kaskazini yadai Marekani na Korea Kusini zinataka kumuua kiongozi wake

Kiongozi wa Korea Kaskazini  Kim Jong Un
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un Reuters/路透社

Korea Kaskazini inadai kuwa serikali ya Marekani na Korea Kusini zinapanga kumuua kiongozi wao Kim Jong-un.

Matangazo ya kibiashara

Wizara ya maswala ya usalama nchini humo imesema mataifa hayo wanatumia kundi la kigaidi linalosaidiwa na shirika la ujasusi la CIA wamepanga mpango huo.

Aidha, Pyongyang inasema mataifa hayo yanapanga kutumia silaha za kibiolojia kumwangamiza kiongozi wao.

Hata hivyo, Korea Kaskazini imesema itahakikisha kuwa inakabiliana na kundi hilo la kigaidi.

Madai haya yameendelea kuzua hali ya wasiwasi katika eneo la Korea.

Marekani na Korea Kaskazini yameendelea kushambuliana kwa maneno huku yakitishiana kushambuliana kwa makombora.

Rais wa Marekani Donald Trump amekuwa akisema kuwa anaweza kukabiliana na Korea Kaskazini hata bila msaada wa China kuhakikisha kuwa haiendelei na mpango wake wa kujaribu silaha za Nyuklia.