MAREKANI-IRAN-USALAMA

Marekani yaongeza vikwazo dhidi ya Iran

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Hassan Rohani, mwaka 2015 katika chumba cha udhibiti wa kituo cha nyuklia cha Bushehr.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Hassan Rohani, mwaka 2015 katika chumba cha udhibiti wa kituo cha nyuklia cha Bushehr. MOHAMMAD BERNO / IRANIAN PRESIDENCY / AFP

Marekani imechukua uamuzi wa kuongeza vikwazo dhidi ya Iran juu ya mpango wake wa utengenezaji wa nyuklia. Rais wa Marekani Donald Trump amesema vikwazo zaidi vinahitajika kupambana na utengenezaji wa silaha za nyuklia duniani.

Matangazo ya kibiashara

Bw Trump amebaini kwamba Marekani itaweka pia vikwazo kwa maafisa pamoja na wafanya biashara kutoka China ambao wanahusishwa na mpango wa nyuklia wa Iran.

Uamuzi huu unakuja licha ya Rais Donald Trump kushutumu sera za mtangulizi wake Barack Obama juu ya kukabiliana na mpango wa nyuklia wa Iran.

Wakati wa kampeni, Donald Trump alitishia kufuta makubaliano yaliyofikiwa kati ya Iran na Marekani kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran ambapo Iran ilikubali kupunguza kiasi chake cha urutubishaji na utengenezaji wa silaha za nyuklia.