MAREKANi-CHINA-USHIRIKIANO-USALAMA

Ndege ya Marekani yakabiliwa na ndege za China

China inaoituhumu Mareani kufanya vitendo vya uchokozi karibu na pwani yake.
China inaoituhumu Mareani kufanya vitendo vya uchokozi karibu na pwani yake. Pilatus Aircraft Ltd - www.pilatus-aircraft.com

Ndege ya Marekani inayohusika na kufanya uchunguzi imezuliwa na ndege mbili za China, kwa mujibu wa taarifa za jeshi la Marekani mapema Ijumaa hii asubuhi.

Matangazo ya kibiashara

China imekuwa ikituhumu vitendo vya Marekani karibu na pwani yake, hatua ambayo imesababisha wasiwasi kati ya mataifa hayo mawili.

“Uzuizi huo haukufanywa kwa njia ya utaalamu kutokana na hali ya rubani wa ndege hiyo ya China ikiwemo kasi ya ndege zote mbil”, msemaji wa jeshi la angani la Marekani Luteni kanali Lori Hodge amesema

“Swala hilo linaangaziwa na China kupitia njia mwafaka ya kidiplomasia mbali na zile za kijeshi”, aliongezea akisema uchungzi wa kijeshi unaendelea.

Ndege hiyo ilikuwa katika safari yake ya kutaka kugundua mionzi katika anga ya kimataifa iliopo mashariki mwa bahari ya China.

Mwezi Februari, ndege moja ya Marekani ilianza kile Washington ilielezea kuwa doria yake ya kawaida kusini mwa bahari ya China ikiandamana na idadi fulani ya meli za kijeshi.

Inaarifiwa kuwa ndege hiyo ilikuwa imetumiwa kugundua ushahidi kuhusu majaribio ya kinyuklia ya Korea Kaskazini.