Rais wa zamani wa Korea Kusini afikishwa mahakamani
Imechapishwa:
Aliyekuwa rais wa Korea Kusini, Park Geun-Hye amefikishwa mahakamani kuanza kesi inayomkabili. Hii ni kwa mara ya kwanza aliye kuwa rais wa nchi hiyo kufikishwa mahakamni mjini Seoul kwa tuhuma za ufisadi.
Pia ni kwa mara ya kwanza Park Geun-Hye kuonekana hadharani tangu kuondolewa mamlakani na kuzuiliwa mwezi Machi mwaka huu.
Hata hivyo Park Geun-Hye amekanusha kufanya makosa yeyote, licha ya tuhuma za ufisadi dhidi ya yake.
Bi Park alifika mahakamani akiongozana na rafiki wake wa karibu, Choi Soon-Sil ambae anatuhumiwa kwa kujipatia fedha kutoka kwa makampuni makubwa.
Park Guen-Hye aliulizwa ajira yake na kujibu hajaajiriwa.