UFILIPINO-USALAMA

Rais wa Ufilipino awaonya wapiganaji wa Kiislam

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte akiyashtumu makundi yta Kiislamu kuzorotesha hali ya usalama kusini mwa Ufilipino.
Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte akiyashtumu makundi yta Kiislamu kuzorotesha hali ya usalama kusini mwa Ufilipino. MANMAN DEJETO / AFP

Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte, ameonya Jumatano hii kuwa atakua makini na kuhakikisha kwamba sheria ya kijeshi inayotumika kusini mwa kisiwa cha Mindanao kuendelea kutekelezwa kwa muda wa mwaka mmoja kama itahitajika.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumanne Rodrigo Duterte alikatikiza ziara yake nchini Urusi na kukiweka kisiwa cha Mindanao chini ya sheria ya kijeshi baada ya mapigano kati ya vikosi vya usalama na wapiganaji wanaohusishwa na kundi la Islamic State.

"Kwa Wananchi wenzangu ambao mnatambua sheria ya kijeshi, si tofauti na kile alichokifanya rais Marcos. Nitakuwa makini kabisa," alisema ndani ya ndege iliokua ikimsafirisha katika mji wa Manila.

"Kwa wananchi wenzangu, msiogope. Narudi nyumbani. Nitashughulikia tatizo hilo mara nitakapowasili."

Askari wawili na polisi mmoja waliuawa na watu kumi na wawili waliuawa katika mji wa Marawi, mji wenye Waislam wengi wa Mindanao ambapo wapignaji wa Kiislam wa kundi la Maute walichukua udhibiti wa majengo kadhaa na kuchoma moto shule, kanisa na gereza.

Sheria ya kijeshi iliwahi kushuhudiwa nchini Ufilipino kwa muda wa muongo mmoja wakati wa utawala wa dikteta Ferdinand Marcos.