JAPAN-KOREA KASKAZINI-USALAMA

Shinzo Abe aituhumu Korea Kaskazini kwa jaribio la makombora

Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe aahidi kuunga mkono makubaliano ya mkutano wa G-7 kuhusu Korea Kaskazini.
Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe aahidi kuunga mkono makubaliano ya mkutano wa G-7 kuhusu Korea Kaskazini. Reuters/路透社

Serikali ya Japan imeishutumu Korea Kaskazini kwa kurusha makombora katika bahari nchini Japan. Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe amesema hivi karibuni katika mkutano wa mataifa yaliostawi kiuchuni (G-7) chokochoko za Korea Kaskazini zilijadiliwa kwa kina.

Matangazo ya kibiashara

Korea Kaskazini imerusha kombora la masafa mafupi, ambalo ni la tatu kurushwa na taifa hilo katika kipindi cha wiki tatu.

Kombora hilo aina ya Scud lilipaa umbali wa kilomita 450 (maili 280) kabla ya kuanguka katika maeneo ya bahari ya Japan, hatua iliyoifanya Japan kulalamika vikali.

“Japan itashirikiana na mataifa mengine ikiwemo Marekani kukabiliana na vitisho vya Korea Kaskazini, “ amesema Shinzo Abe.

Waziri Mkuu wa Japan ameahidi kuunga mkono makubaliano ya mkutano wa G-7.

Korea Kaskazini imeendelea kukiuka azimio la Umoja wa Mataifa linaloizuia kufanya majaribio yoyote ya makombora au silaha za nyuklia, na imeongeza kasi na idadi ya majaribio hayo katika miezi ya karibuni.

Kikosi cha Jeshi la Marekani Bahari ya Pasifiki kimesema kombora hilo lilirushwa kutoka Wonsan, Korea Kaskazini na lilipaa kwa karibu dakika sita kabla ya kuanguka.

Msemaji wa jeshi la Korea Kusini amesema kombora hilo lilipaa juu hadi kilomita 120 angani, na utathmini unaendelea kubaidi "idadi hasa ya makombora yaliyorushwa," ishara kwamba huenda nchi hiyo ilirusha zaidi ya kombora moja.

Jariibo hilo la kombora limetekelezwa siku moja baada ya vyombo vya habari vya serikali nchini Korea Kaskazini kusema nchi hiyo ilifanyia majaribio mfumo mpya wa kudungua ndege za kivita, na kutoa picha za kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un alishuhudia majaribio hayo.