URUSI-HALI YA HEWA

Kimbunga chaua watu kadhaa Moscow

Dhoruba lioikumba mji wa Moscow iling'oa miti na kuharibu magari.
Dhoruba lioikumba mji wa Moscow iling'oa miti na kuharibu magari. REUTERS/Andrey Kuzmin

Dhoruba kubwa ambayo haijawahi kushuhudiwa katika mji mkuu wa Urusi, Moscow, ilipiga mji huo siku ya Jumatatu, Mei 29 mchana na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 13.

Matangazo ya kibiashara

Mamlaka ya hali ya hewa nchini Urusi haikuweza kupata taarifa ya hali hiyo katika mji wa Moscow. Hata hivyo kimbunga hiki hakikudumu kwa muda mrefu, lakini kilisababisha hasara kubwa. Kuelekea saa 9 alaasiri, mvua kubwa zilinyesha, na upepo wa mita 22 kwa sekunde, sawa na kasi ya kilomita 80 kwa saa ulipiga mji huo.

Maelfu ya miti iling'olewa, paa za nyumba ziliruka na kuharibiwa vibaya, magari kadhaa yalipelekwa na maji.

Maafisa wa usalama wanasema watu wasiopungua 13 walipoteza maisha. Watu waliojeruhiwa walisafirishwa hospiotalini na katika vituo vya afya. Kimbunga kibaya kuwahi kutokea katika mji wa Moscow ni kile cha tarehe 21 Juni, 1998 na kiliua watu 9 na kuwajeruhi wengine 165.

Nyaya za umeme zilianguka na kuacha zaidi ya watu 7 000 bila umeme. Usafiri ulisitishwa, vituo kadhaa vya treni vilifungwa na safari za ndege zilisitishwa. Hali hii ya hewa piailisababishwa watu kuchelewa katika vituo vya treni na viwanja vya ndege, lakini hakuna haikusababisha hasara kubwa katika maeneo mengine nje ya mji huo.