BANGLADESH-USALAMA

Maelfu ya watu pwani ya Bangladesh wahamishwa kufuatia kimbunga Mora

Maofisa wa serikali wanakema wana hofu kuwa huenda kimbunga Mora kikasababisha hasara kubwa kama watu hawata kuwa makini na viongozi tawala kuchukua hatua za tahadhari.
Maofisa wa serikali wanakema wana hofu kuwa huenda kimbunga Mora kikasababisha hasara kubwa kama watu hawata kuwa makini na viongozi tawala kuchukua hatua za tahadhari. REUTERS/Mohammad Ponir Hossain

Maelfu ya wakazi wa pwani ya Bangladesh wametakiwa kuhama na kwenda maeneo salama saa chache ya kimbunga chenye nguvu kuonekana kuelekea katika maeneo hayo. Maeneo kadhaa ya pwano hiyo yamewekwa kwenye hali ya hatari.

Matangazo ya kibiashara

Maofisa wa serikali wanasema wanatarajia kuhamisha zaidi ya watu nusu mulioni kwenda katika maeneo ambayo wanaona kama kimbuga hiki hakitafika.

Kimbunga hiki kinachojulikana kwa jina la Mora kinatarajiwa kusababisha maafa makubwa wakati ambapo maafisa wakitaka juhudi zaidi kufanyika ikiwemo kuongeza boti za uokoaji.

Maduka, ofisi mbalimbali zimefungwa huku shughuli zimesimamishwa kufuatia kimbiunga hiki. Maelfu ya watu wameanza kujielekeza katika maeneo salama, huku maofisa wa serikali wakisema wana hofu kuwa huenda kimbunga hiki kikasababisha hasara kubwa kama watu hawatakuwa makini na viongozi tawala kuchukua hatua za tahadhari.