UFILIPINO-USALAMA-MAPIGANO

Wapiganaji 89 wa Kiislam wauawa katika muda wa siku tisa nchini Ufilipino

Askari wa Ufilipino akiwa katikakifaru cha kijeshi katika mji wa Marawi katika kisiwa cha Mindanao, Mei 30, 2017.
Askari wa Ufilipino akiwa katikakifaru cha kijeshi katika mji wa Marawi katika kisiwa cha Mindanao, Mei 30, 2017. AFP

Vikosi vya usalama vya Ufilipino vimewaua wapiganaji 89 wa Kiislam kwa muda wa zaidi ya wiki moja ya mapigano katika mji ulio kusini mwa Ufilipino, ambapo baadhi ya vitongoji bado vinashikiliwa na wapiganaji, jeshi la Ufilipino limetangaza Jumatano hii Mei 31.

Matangazo ya kibiashara

Helikopta za kijeshi zimeku zikiendelea Jumatano hii asubuhi kurusha roketi ngome za wapiganaji hao katika mji wa Marawi, mji wenye Waislamu wengi katika kisiwa Wakatoliki wengi.

Wapiganaji wa Kiislamu, awanaoadai kuwa wa kundi la Islamic State (IS) wanaendelea kuwashikilia mateka, wakati ambapo maelfu ya raia walikuwa wamekwama kwa mapigano.

Mapigano yalizuka baada ya mashambulizi ya angani ya vikosi vya usalama dhidi ya maficho yanayodhaniwa kuwa ya Isnilon Hapilon, anaechukuliwa kama kiongozi wa IS nchini Ufilipino.

Marekani imetenga kitita cha Dola 5 milioni (sawa na Euro milioni 4.5) kwa atakaemuua au kumkamata kiongozi huyo wa IS. Isnilon hapilon pia ni mmoja wa viongozi wa kundi la Abu Sayyaf, kundi linalojihusisha na tabia ya utekaji nyara.

Isnilon Hapilon pengine bado yupo katika mji wa Marawi, msemaji wa jeshi, Restituto Padilla amewaambia Jumatano hii waandishi wa habari, na kuongeza kuwa vikosi vya usalama vimemewaua wapiganaji 89 wa Kiislam.