UFILIPINO-USALAMA

Watu 36 wauawa katika shambulio dhidi ya hoteli Resorts World Manila

Wakazi na wafanyakazi wa Hoteli Resorts World Manila ilioshambuliwa wasimama nje ya jengo la hoteli hiyo,Manila, Juni 2, 2017.
Wakazi na wafanyakazi wa Hoteli Resorts World Manila ilioshambuliwa wasimama nje ya jengo la hoteli hiyo,Manila, Juni 2, 2017. REUTERS/Erik De Castro

Miili thelathini na sita ya watu waliouawa imegunduliwa leo Ijumaa Juni 2 katika katika hoteli Resorts World Manila casino ilioshambuliwa na mtu aliyejihami kwa silaha kabla ya kujiua. Polisi katika mji wa Manila inasema kwamba mtu ambaye alitekeleza shambulizi hilo pengine ni raia wa kigeni.

Matangazo ya kibiashara

"Watu thelathini na sita wameuawa," alisema kwenye kituo cha CNN nchini Ufilipino mkuu wa polisi ya mji wa Manila, Oscar Albayalde baada ya shambulio hilo lililotokea usiku kuamkia leo Ijumaa katika hoteli Resorts World Manila, hoteli inayopatikana karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa katika mji mkuu wa Ufilipino, Manila. Awali afisa mwengine wa polisi, Tomas Apolinaro alisema watu 34 waliuawa katika shambulio hilo.

Polisi wanasema kuwa, mtu aliyekuwa amejihami kwa silaha alivamia ukumbi wa Casino katika jiji hilo na kuanza kuwapiga watu risasi.

Aidha, wanasema mtu ambaye alitekeleza shambulizi hilo alijiuawa kwa kujipiga risasi baada ya kuanza kukabiliana na maafisa wa usalama.

Ripoti zinasema kuwa, watu wengi walipoteza maisha baada ya kuathiriwa na moshi katika ukumbi huo baada ya kushika moto kutokana na makabiliano hayo.

Watu zaidi ya 50 wamejeruhiwa katika shambulizi hili ambalo linachunguzwa kama la kigaidi au kama ni uhalifu wa kawaida uliofanyika.