MANILA-USALAMA

Shambulizi la Casino mjini Manila halikuwa la kigaidi;polisi

Raisi wa Ufilipino Rodrigo Duterte
Raisi wa Ufilipino Rodrigo Duterte Reuters/路透社

Mwanaume aliyewasha moto katika Casino mjini Manila nchini Ufilipino na kuua watu 37 ametambulika kama baba wa watoto watatu mwenyeji wa Manila ambaye alichochewa na madeni ya kamari na sio ugaidi polisi imefahamisha.

Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa polisi mjini Manila Oscar Albayalde amethibitisha kuwa tukio hilo halikuwa la kigaidi bali ni tukio la mtu mmoja aliyeamua kufany auhalifu.

Albayalde ameeleza kuwa mwanaume aliyetambulika kama Jessie Carlos, 43, muumini wa Kanisa la Catholic na baba wa watoto watatu alikuwa amepigwa marufuku kuingia katika casino yoyote mnamo mwezi April kutokana na familia yake kutoridhia mtu huyo kujihusisha na kamari.

Kwa mujibu wa familia kutokana na vitendo vya mwanaume huyo amekuwa akisababisha migogoro ndani ya familia yake.

Mwanaume huyo aliyejificha sura alivamia casino moja mjini Manila siku ya ijumaa akiwa na silaha ya moto na chupa yenye mafuta ya Petroli kabla ya kuwasha moto katika vyumba tofauti vya jengo hilo.