BURMA-USALAMA

Miili na mabaki ya ndege ya Myanmar yapatikana baharini

Jeshi la Burma limetangaza kwamba mabaki ya ndege ya jeshi iliyotoweka ikiwa na watu 122 yamepatikana. Ndege hiyo ilikuwa safarini kutoka Myeik ikielekea Yangon.

Askari wa Myanmar wakipiga doria katika kijiji cha  Maungdaw katika jimbo la Rakhine kwa kukabiliana na makundi ya wapiganaji wa Kiislam.
Askari wa Myanmar wakipiga doria katika kijiji cha Maungdaw katika jimbo la Rakhine kwa kukabiliana na makundi ya wapiganaji wa Kiislam. STR / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mabaki ya ndege na maiti zimepatikana katika bahari ya Andaman, kwa mujibu wa taarafa ya jeshi la Burma.

Ndege hiyo ilikuwa imefanya safari ya nusu saa wakati ilipoteza mawasiliano siku ya Jumatano

Ndege hiyo aina ya Y8 iliyotengezwa nchini China ilikuwa na wahudumu 14 pamoja na wanajeshi 106 na familia wakiwemo watoto.

Ndege hii ilinunuliwa China mwezi Machi mwaka uliopita na tayari ilikuwa imeruka kwa saa zaidi ya 800.

Myanmar imeendelea kukumbwa na ajali za ndege miaka ya hivi karibuni. Ajali zaidi ya tatu zilishuhudiwa nchini humo na kusababisha vifo vya watu wengi. Mwezi Februari mwaka 2016 watu watano waliokuwa wakisafiri wakitumia ndege ya jeshi walifariki wakati ndege hiyo ilianguka kwenye mji mku wa Nay Pyi Taw.