MAREKANI-KOREA KASKAZINI-HAKI

Warmbier afariki baada ya kuachiwa nchini Korea Kaskazini

Otto Frederick Warmbier, alipokua mbele ya mahakama mjini Pyongyang, Februari 29, 2016.
Otto Frederick Warmbier, alipokua mbele ya mahakama mjini Pyongyang, Februari 29, 2016. REUTERS/Kyodo

Mwanafunzi mwenye asili ya Marekani, Otto Warmbier, aliyeachiwa huru hivi karibuni nchini Korea Kaskazini na kurejeshwa nchini Marekani siku saba zilizopita, amefariki dunia. Otto Warmbier alishikiliwa kizuizini miezi kumi na mitano nchini Korea Kaskazini.

Matangazo ya kibiashara

Familia yake imeinyooshea kidole cha lawama Korea Kaskazini kufuatia kifo hicho, ikisem akuwa kifo hicho kimesababishwa na unyanyasaji mkali dhidi ya kijana wao aliokuwa akikabiliana nao alipokuwa mikononi mwa maofisa usalama wa Korea Kaskazini .

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba Otto Warmbier alikabiliana na mazingira magumu akiwa nchini humo, huku akisem akuwa utawala wa Korea Kaskazini ni wa ukatili mkubwa na hauheshimu haki yoyote ya kibinadamu.

Donald trump amesema Otto Warmbier alikuwa katika hali ya kutojitambua alipoachiliwa kutoka jela.

Itafahamika kwamba baada ya kuachiwa, Otto Warmbier alilazwa hospitalini kwa matibabu zaidi karibu na nyumbani kwake mjini Cincinnati.

Madaktari waliokuwa waliokua wakimuhudumia Warmbier wamesema kwamba alikuwa na majeraha makubwa.