MAREKANI-CHINA-USHIRIKIANO

Donald Trump: Marekani ina uhusiano mzuri na China

Rais Donald Trump ameitaka China kuikanya Korea Kaskazini.
Rais Donald Trump ameitaka China kuikanya Korea Kaskazini. REUTERS/Kevin Lamarque

Rais wa Marekani Donald Trump kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema serikali yake ina uhusiano mzuri sana na China. Aidha, amesema kuwa anaukubali sana uongozi wa rais Xi Jinping.

Matangazo ya kibiashara

Kuali hii ya Trump imekuja siku moja baada ya kiongozi huyo wa Marekani kusema kuwa China ilishindwa kuizua mshirika wake wa karibu Korea Kaskazini kuachana na majaribio ya silaha zake za nyuklia.

Rais Donald Trump ameitaka China kuikanya Korea Kaskazini kuachana na mpango wake wa kutengeneza silaha za nyuklia na mpango wake wa kurusha makombora ya masafa marefu.

Wakati huohuo Waziri wa mMashaiuriano ya kigeni wa Marekani Rex Tillerson ameyataka mataifa yote kuongeza juhudi za kumaliza biashara ya kihalifu ya Korea Kaskazini ambayo anasema inatumika kufadhili mipango yake ya Kinyuklia

Akizungumza baada ya kukutana na maafisa wakuu wa China, waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson amesema kuwa Beijing ina jukumu la kidiplomasia kuongeza shinikizo zaidi kwa Pyongyang iwapo ingetaka kupunguza wasiwasi katika eneo hilo.