KOREA KASKAZINI-MAREKANI

Korea Kaskazini yamwita Trump "mwenda wazimu"

Kiongozi wa Korea Kaskazini  Kim Jong-Un
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un KCNA/ via REUTERS

Korea Kaskazini imesema rais wa Marekani Donald Trump ni mtu aliye na matatizo ya akili (Mwenda wazimu), kipindi hiki wasiwasi ukiendelea kushuhudiwa kati ya nchi hizo mbili.

Matangazo ya kibiashara

Kauli hii inakuja siku moja baada ya rais Trump kulaani Korea Kaskazini kwa kuhusika na kifo cha raia wake Otto Warmbier.

Waimbier alirejea nyumbani wiki iliyopita akiwa kama hali mahututi kuja kupewa matibabu baada ya kuzuiwa na kuteswa kwa muda mrefu.

Raia huyo wa Marekani alikuwa Mwanafunzi nchini Korea Kaskazini na alipewa kifungo cha miaka 15 jela kwa madai ya kusambaza propaganda.

Gazeti la serikali ya Korea Kaskazini Rodong Sinmun limemshutumu Trump kuingilia maswala ya nchi hiyo wakati akiendelea kupitia wakati mgumu katika nchi yake.

Trump na uongozi wa Korea Kusini umeshtumu uongozi wa Pyongyang kuwa wa kidikteta.