CHINA

Matumaini ya kupata manusura zaidi yafifia siku 2 baada ya maporoko ya ardhi nchini China

Maporomoko ya Ardhi Kusini Magharibi mwa China
Maporomoko ya Ardhi Kusini Magharibi mwa China RFI/Portuguese

Matumaini ya kupata manusura wengine baada ya kutokea kwa maporomoko ya ardhi Kusini magharibi mwa China yanazidi kufifia wakati huu idadi ya watu ambao bado hawajulikani walipo ikitajwa kuwa 118

Matangazo ya kibiashara

Waokozi wamefanikiwa kupata miili 15 kutoka kwenya mabaki ya miamba iliyoafunika nyumba 62 huko Xinmo , kijiji chenye milima kilicho jirani na mto jimboni Sichuan.

Maporomoko hayo ya ardhi yaliyotokea majira ya asubuhi siku ya Jumamosi na yanaaminika kuchochewa na mvua kubwa .

Manusura watatu pekee mtu na mkewe na mtoto wao wa mwezi mmoja , ndio wamepatikana wakiwa hai tangu mvua kubwa kusababisha kuanguka kwa upande mmoja wa mlima mapema jana Jumamosi.