URUSI-UKRAINE-URUSI-USALAMA

Makampuni mengi duniani yashambuliwa kimtandao

Baada ya kuyakumba baadhi ya makampuni ya Ukraine na Urusi, mashambulizi ya kimtandao yalisambaa Ulaya ya Magharibi.
Baada ya kuyakumba baadhi ya makampuni ya Ukraine na Urusi, mashambulizi ya kimtandao yalisambaa Ulaya ya Magharibi. REUTERS/Kacper Pempel/Illustration/File Photo

Mashambulizi makubwa ya udukuzi yalianza kuyakumba baadhi ya makampuni siku ya Jumanne, Juni 27 nchini Urusi na Ukraine kabla ya kusambaa katika makampuni mengi duniani.

Matangazo ya kibiashara

Kampuni kubwa ya mafuta ya Rosneft imeathiriwa na mashambulizi haya, ikiwa ni pamoja na kampuni ya Saint-Gobain ya Ufaransa na kampuni ya madawa ya Marekani ya Merck.

Kompyuta za kituo kikuu cha nyuklia cha Tchernobyl pia kimeshambuliwa. Mashambulizi haya yanakumbusha mashambulizi ya virusi viliopewa jina la WannaCry vilioathiri maelfu ya kompyuta kote duniani mwezi uliopita.

Kampuni ya Urusi ya Group-IB yaenye utaalamu wa usalama wa maswala ya kompyutainaeleza makampuni 80 yaliolengwa nchini Urusi na Ukraine na mashambulizi haya makubwa ya udukuzi wa mitandao yaliyotokea siku ya Jumanne Juni 27. Miongoni mwa makampuni hayo, ni pamoja na kampuni kubwa ya mafuta ya Rosneft ya Urusi, benki kuu na miundo ya serikali Ukraine, lakini pia kituo kikuu cha nyuklia cha Chernobyl.

Madhara makubwa yalishuhudiwa kufuatia mashambulizi hayo. Benki ya taifa ya Ukraine ilisema katika taarifa yake kwamba "benki nyingi zilipata usumbufu kwa kuwahudumia wateja wao." Kwenye ukurasa wake wa Facebook, shirika la reli lilisema kuwa haliweza kukubali malipo ya kadi ya benki katika vituo vyake vya kulipia. Wakati huo huo mamlaka ya uwanja wa ndege wa mji mkuu wa nchi hiyo ilisema tovuti rasmi na mabango ya kuonyesha safari za ndege kwenye uwanja wa ndege wa Borispol, isipokuwa uwanja mmoja pekee wa ndege, ulishindwa kufanya shughuli zake na kubaini kwamba safari za ndege zinaweza kuchelewa. Tovuti ya serikali ya Ukraine pia ilikumbwa na matatizo mchana.

Nchini Marekani, kampuni ya madawa ya Merck kwa upande wake ilibaini kwamba ilikumbwa na mashambulizi hayo. "Mfumo wetu wa mambo ya kompyuta umekumbwa na mashambulizi ya udukuzi wa mtandao duniani," msemaji mmoja ameliambia shirika la habari la AFP, na kuongeza kwamba kampuni hiyo iligundua udukuzi wa mtandao mapema mchana katika ukanda wa pwani ya Marekani ya Mashariki.

Kwa mujibu wa shirika la usalama wa maambo ya kompyuta (ANSSI), "mashambulizi yameanza kupatiwa ufumbuzi ili kuelewa kinachoendelea katika masuala ya kiufundi, na kuchapisha mapendekezo jioni. "