SREBRENICA-MAUAJI-USALAMA

Uholanzi yahusika katika mauaji ya kimbari Srebrenica

Asasi ya Akina mama wa Srebrenica, ambalo wanachama walikuwa mjini Hague Jumanne Juni 27 wamekata tamaa kufuatia uamuzi wa Mahakama ya Rufaa, ambayo imeinyoosheshe kidole cha lawama Uholanzi kuhusika kwa sehemu moja kwa vifo vya waislamu wa Bosnia1995 laki
Asasi ya Akina mama wa Srebrenica, ambalo wanachama walikuwa mjini Hague Jumanne Juni 27 wamekata tamaa kufuatia uamuzi wa Mahakama ya Rufaa, ambayo imeinyoosheshe kidole cha lawama Uholanzi kuhusika kwa sehemu moja kwa vifo vya waislamu wa Bosnia1995 laki Remko de Waal / ANP / AFP

Mahakama ya Rufaa ya Uholanzi imebaini siku ya Jumanne Juni 27, 2017 kwamba serikali ya nchi hiyo ilihusika kwa sehemu moja kwa vifo vya mamia ya waathirika wa mauaji ya kimbari ya Srebrenica katika majira ya joto 1995.

Matangazo ya kibiashara

Askari wa uholanzi hangepaswa, kwa mujibu wa mahakama kukabidhi kwa vikosi vya Bosnia na Serbia wakimbizi waliokua wakilindwa na askari wa Dutchbat, bataliani ya askari wa ulinzi wa Umoja wa Mataifa kutoka Uholanzi (UNPROFOR).

Kwa ujumla, wananchi 8,000 wa Bosnia - wanaume, vijana na wazee - waliuawa katika mauaji ya kimbari dhidi ya Waislamu wa Bosnia, wakati eneo la Srebrenica lilidhibitiwa Julai 1995. Uamuzi wa Mahakama ya Rufaa ya Hague ulibaini kwamba watu 350 ndio waliouawa katika mauaji hayo, mwandishi wetu Pierre Benazet, amearifu.

Watu hawa 350 ni wale ambao walibaki mwisho katika eneo ambalo askari wa kulinda amani kutoka Uholanzi walipaswa kulinda. familia zao zilifungua mashitaka na katika uamuzi wa mahakama ya mwanzo mwaka 2014, mahakama ilibaini kwamba chi ya Uholanzi ilihusika kwa vifo hivyo.

Hatimaye, kuhusika huko kumethibitisha kwa sababu kwa mujibu wa Mahaka ya Rufaa ya Hague, askari wa bataliani ya Dutchbat hawangeweza kupuuzia hatari kwamba vikosi vya Waserbia wa Bosnia vilikua vikiwalenga watu hao kutoka Bosnia. Mahakama imebaini kwamba "serikali ya Uholanzi ilifanya kitendo hicho kinyume cha sheria."

Askari wa Uholanzi, waliojificha katika kambi yao, waliwakusanya maelfu ya wakimbizi katika eneo la Umoja wa Mataifa, lakini kufuatia wingi wa wakimbizi hao, askari wa Uholanzi walifungia milango kwa nje wakimbizi waliokua wakiwasili kwa wingi. Kisha waliwaruhusuvikosi vya Waserbia wa Bosnia kuwahamisha wakimbizi hao. Wanaume na wavulana walitenganishwa na kuwekwa katika mabasi.

Vikosi vya Umoja wa Mataifa kutoka Uholanzi "waliwezesha mgawanyo wa wanaume Waislamu na wavulana, huku wakijua kuwa kulikuwa na hatari kwamba watafanyiwa mateso au kuuawa na Waserbia wa Bosnia," alisema jaji wa mahakama, Gepke Dulek.