MAREKANI-URUSI-USHIRIKIANO

Donald Trump kukutana na Vladimir Putin wiki ijayo

Ikulu ya White House yathibitisha uwepo wa mkutano kati ya Donald Trump na Vladimiri Putin wiki ijayo..
Ikulu ya White House yathibitisha uwepo wa mkutano kati ya Donald Trump na Vladimiri Putin wiki ijayo.. REUTERS/Carlos Barria

Rais wa Marekani Donald Trump atakutana na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin wiki ijayo, kwa mujibu wa Ikulu ya Marekani. Mkutano wa viongozi hawa ni maandalizi ya mkutano wa nchi 20 zilizoendelea zaidi kiuchumi duniani (G20).

Matangazo ya kibiashara

Mshauri wa masuala ya ulinzi wa Marekani H.R. MacMaster amesema bado haijafahamika mada maalumu itakayozungumziwa katika mkutano wa wawili hao.

Mapema wiki hii ikulu ya Kremlin kupitia msemaji wake, ilithibitisha mkutano huo.

Itakua ni mara ya kwanza rais Donald Trump kukutana uso kwa uso na mwenzake wa Urusi Donald Trump.

Viongozi hawa wawili wanakutana, wakati ambapo rais wa Marekani anaendelea kukabiliwa na ukosoaji mkubwa kufuatia kuzuka kwa shutma kwamba maafisa wake walitoa siri za ndani za Marekani kwa Urusi kabla ya kuchaguliwa kwake kuingoza Marekani mwaka uliopita.