CHINA-MAREKANI-USHIRIKIANO

China yailaumu Marekani kupitisha manowari yake karibu na kisiwa chake

Meli yaUSS Stethem inayodaiwa na china kupita karibu na kisiwa kinachozozaniwa kusini mwa bahari ya China.
Meli yaUSS Stethem inayodaiwa na china kupita karibu na kisiwa kinachozozaniwa kusini mwa bahari ya China. Wikipédia

China imeishtumu Marekani kwa hatua yake yakupitisha manowari yake karibu na kisiwa kinachozozaniwa kusini mwa bahari ya China, na kubaini kwamba hatua hiyo ni uchokozi mbaya. Kisiwa hicho kidogo pia kinadaiwa na Vietnam na Taiwan.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo China imesema kuwa itafanya kila iwezalo kulinda usalama wake, huku ikijibu kwa kutuma meli za kijeshi na ndege kuenda kisiwa hicho.

Manowari ya USS Stethem ilipita karibu na kisiwa kinachozozaniwa cha Triton ambacho ni moja ya visiwa vinavyodaiwa na China na nchi zingine, hususan Japan.

Kisa hiki kilitokea muda kabla ya viongozi wa nchi hizo mbili kufafanya mazungumzo ya simu.

China imekuwa kwenye mzozo wa umiliki wa maeneo ya bahari na majirani zake kadha miaka ya hivi karibuni.

Hivi karibuni Marekani iliionya China kutoakana na uamuzi wake wa kuendelea kujipa kwa mabavu visiwa katika maeneo yanayozozaniwa. Cina imefutilia mbali onyo hilo na kusma kwamba inafanya hivyo kwa kulinda haki zake.

China imekua ikiilaumu Marekani kwa kuchochea vurugu eneo hilo, ikisem aMarekani ina hasira kwa kuwa uhusiano kati ya China na majirani zake umeimarika.

China imekuwa kwenye mzozo wa umiliki wa maeneo ya bahari na majirani zake kadha miaka ya hivi karibuni.