BURMA-USALAMA

Watu kutoka jamii ya Rohingya waendelea kuikimba Burma

Wakimbizi wa Warohingya wanasubir iboti baada ya kuvuka mpaka kati ya Burma na Bangladesh, Septemba 7 2017.
Wakimbizi wa Warohingya wanasubir iboti baada ya kuvuka mpaka kati ya Burma na Bangladesh, Septemba 7 2017. REUTERS/Mohammad Ponir Hossain

Serikali ya Myanmar imesema kuwa inafanya kila linalowezekana kuhakikisha Waislamu wa jamii ya Rohingya inalindwa.

Matangazo ya kibiashara

Licha ya kutozungumzia moja kwa moja wimbi la wakimbizi la wakimbizi Waislamu wa jamii ya rohingya Kiongozi wa Myanmar Aung San Suu Kyi alisema jana kuwa serikali yake inafanya kila linalowezekana kumlinda kila mtu katika jimbo linalokabiliwa na machafuko la Rakhine,

Mashirika ya kimisaada yanaripoti kuwa idadi ya Wakimbizi hao inaendelea kuongezeka siku baada ya siku baadhi wakiwa wanyonge kutokana na safari ngumu katiuka mazingira hatarishi.

Bangladesh imesema takribani Warohingya waliokimbilia nchini ikifikia 164,000.

Suu Kyi hakuzungumzia moja kwa moja wimbi la Warohingya wanaokimbia ambalo lilisababishwa na mashambulizi ya wanamgambo mnamo terehe 25 mwezi uliopita na operesheni ya jeshi kuwakabili, lakini akasema utawala wake unajitahidi kuwalinda raia.

Wakosoaji katika nchi za Magharibi wamemtuhumu Suu Kyi kwa kutowatetea Warohingya na baadhi yao wametaka tuzo ya amani ya Nobel aliyoshinda mwaka 1991 kama shujaa wa demokrasia ifutiliwe mbali.

Wakati haya yakiarifiwa waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu amejumuika na mwenzake wa Bangladesh Abul Hassan Mahmood Ali, kuzitembelea kambi za muda za maelfu ya Warohingya nchini Myanmar.