BURMA-MAUAJI-USALAMA

Umoja wa Mataifa kukutana kuhusu wakimbizi wa Rohingya

Umoja wa Mataifa unatiwa wasiwasi na udhalimu unaofanyiwa watu kutoka jamii ya Rohingya, nchini Myanmar.issement de nouvelles sanctions contre la Corée du Nord, ce mercredi 2 mars 2016.
Umoja wa Mataifa unatiwa wasiwasi na udhalimu unaofanyiwa watu kutoka jamii ya Rohingya, nchini Myanmar.issement de nouvelles sanctions contre la Corée du Nord, ce mercredi 2 mars 2016. REUTERS/Brendan McDermid

Jumuiya ya Kimataifa inashuhudia mgawanyiko mkubwa wakati huu nchi wanachama wa baraza la usalama la umoja wa Mataifa zikitarajiwa kukutana kujadili janga la wakimbizi nchini Myanmar huku nchi ya China ikiunga mkono operesheni za jeshi la nchi hiyo zinazokosolewa na Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Hatua ya China kuonesha kutounga mkono matamshi ya Marekani inamaanisha kuwa huenda baraza la usalama likashindwa kuruhusu kufanyika kwa tathmini ya karibu kuhusu maelfu ya wakimbizi wa Rohingya wanaokimbilia nchini Bangladesh kutokea Myanmar.

Hivi karibuni ofisi za shirika la Umoja wa mataifa linalohusika na mikakati ya ugavi wa misaada OCHA ilifahamisha kuwa idadi ya wakimbizi kutoka Myanmar imefikia watu 370,000.

Umoja wa Mataifa chini ya ripoti iliotolewa na shirika la OCHA umefahamisha kuwa idadi ya wakimbizi kutoka jamii ya Rohingya walioondoka Myanmar imefikia watu 370,000 nchini Bangladesh.

Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi Dunia Aslam Khan alifanya mkutano na waandishi wa habari ikishirikiana na Leonard Doyle mjini Geneva kuhusu wakimbizi wa Rohingya Bangladesh.

Mashirika ya kimisaada yanaripoti kuwa idadi ya Wakimbizi hao inaendelea kuongezeka siku baada ya siku baadhi wakiwa wanyonge kutokana na safari ngumu katiuka mazingira hatarishi.

Mwishoni mwa wiki iliyopita serikali ya Myanmar ilisema kuwa inafanya kila linalowezekana kuhakikisha Waislamu wa jamii ya Rohingya inalindwa.