Wakimbizi wa Rohingya wazuiwa kuhama maeneo nchini Bangladesh
Imechapishwa:
Bangladesh hapo jana imezuia kuhama kwa wakimbizi wa Rohingya, katika maeneo ambayo wamepangiwa na serikali hasa maeneo ya mpaka ambapo zaidi ya wakimbizi laki nne ambao wamekimbia vurugu nchini Myanmar wanaishi katika mazingira magumu.
Hatua hizo ngumu zimechukuliwa wakati huu Dhaka ikijitahidi kukabiliana na kiwango cha mgogoro usio wa kawaida huku Waziri Mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina akijielekeza kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuomba msaada wa kimataifa.
Idadi ya wakimbizi wa Rohinya wanaokimbilia Bangladeshi kutokana na mapigano nchini Myanmar imefika laki nne (400,000).
Waziri mkuu huyo ameondoka siku moja baada ya serikali yake kumwita mjumbe wa Myanmar kwa mara ya tatu kupinga vitendo vinavyofanywa na nchi hiyo jirani yake.