KOREA KASKAZINI USALAMA

Kim Jong-un amjibu Donald Trump

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amjibu Donald Trump baada ya rais huyo wa MArekani kuitisha Kora Kaskazini kwamba ataisambaratisha.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amjibu Donald Trump baada ya rais huyo wa MArekani kuitisha Kora Kaskazini kwamba ataisambaratisha. KCNA via REUTERS

Vita vya maneno kati ya Korea ya Kaskazini na Marekani vinaendelea. Katika taarifa isiyo ya kawaida ya Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alijibu moja kwa moja kwa mwenzake wa Marekani Donald Trump, ambaye wiki hii katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa alitishia Korea Kaskazini kwa "kuisambaratisha."

Matangazo ya kibiashara

Jibu la Korea Kaskazini linaonyesha hali nzito ya baadaye kutoka Pyongyang.

"Trump alinitusi mimi na nchi yangu, ulimwengu ukishuhudia, " amesema Kim Jong-un maneno ambayo yalichapishwa katika gazeti la kila siku la serikali ya Pyongyang.

Kim jong-un aliitwa na Donald Trupm "mtu mwenye mawazo ya kutishia usalama ulimwengu". Kim Jong-un ametishia "kumtibu kwa moto rais wa Marekani mwenye ugonjwa wa akili". "Badala ya kuniogopesha, [vitisho vya Trump] vimenionyesha kwamba njia niliyochagua ni sahihi na kwamba ni lazima niifuate hadi mwisho," ameongeza Kim Jong-un, ambaye ameahidi kulipiza kisasi "kwenye ngazi ya juu".

Wakati wa ziara yake mjini New York kwa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini alisema ulipizaji kisasi unaweza kuwa jaribio la bomu la hidrojeni katika Bahari ya Pasifiki. Hali inayoonyesha tishio la kipekee na kubwa.

Vita hivi vya maneno vinaonyesha kwamba ubabe wa Donald Trump katika Umoja wa Mataifa ni kinyume kabisa.

Onyo jingine la Marekani

Masaa machache baada ya kutangaza vikwazo vipya vya kiuchumi dhidi ya Korea ya Kaskazini, mwandishi wetu mjini New York, Marie Bourreau, amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Rex Tillerson aliomba Baraza la Usalama Umoja wa Mataifa kutuma ujumbe kwa Kim Jong-un. "Korea ya Kaskazini inaelezea kwamba silaha za nyuklia zitahakikisha kuwepo kwa utawala wake; kwa kweli, silaha za nyuklia zitaipelekea nchi hiyo kuzidi kutengwa. "