UN-KOREA KASKAZINI-USALAMA

Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa: Mgogoro wa Korea Kaskazini kutawala mazungumzo

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, wakati wa uzinduzi wa jaribio la kombora la Hwasong-12 tarehe 16 Septemba 2017.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, wakati wa uzinduzi wa jaribio la kombora la Hwasong-12 tarehe 16 Septemba 2017. KCNA via REUTERS

Baada ya kauli kali dhidi ya nchi za Kikomunisti siku ya Jumatano Septemba 19 katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Donald Trump alitangaza siku ya Alhamisi kuweka vikwazo vipya dhidi ya nchi hizo.

Matangazo ya kibiashara

Vikwazo hivyo vinalenga sekta ya nguo, uvuvi, teknolojia ya habari na sekta za viwanda. Hatua zilizopangwa kushinikiza nchi hizo kuachana na mipango yao ya nyuklia na majaribio ya makombora ya masafa marefu. Mgogoro wa Korea Kaskazini pia ulitawala mazungumzo na vikao vyasiku ya Alhamisi katika mkutano Mkuu wa Umoja w Mataifa.

Ni njia gani nzuri zaidi ya kuweka shinikizo kwa Korea ya Kaskazini? Suala hili bado linagawanisha wahusika wa mgogoro huo, Marekani upande mmoja na upande mwingine washirika wa karibu wa serikali ya Pyongyang, China na Urusi, amearifu mwandishi wa RFI mjini New York, Achim Lippold.

Wakati ambapo Washington imepitisha hatua kali, Moscow imeonya uwezekano wowote wa kutumia nguvu za jeshi. "Ongezeko la mapambano linaendelea kushuhudiwa kwenye rasi ya Korea. Tunalaani vikaliharakati za kijehi na mpango wa nyuklia wa Pyongyang, ambavyo ninakiuka maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Lakini kuongezeka kwa mazoezi ya kijeshi karibu na Korea Kaskazini ni kutaka kusababisha janga. Maazimio yote ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yanapaswa kutekelezwa, ni jambo ambalo halina hoja. Hata hivyo, maazimio haya yote yanaendana na vikwazo, hatua inayopelekea kuewepo na haja ya kurudi kwenye meza ya mazungumzo. Tunaita Korea Kaskazini kuacha kuzuia mikataba hii. Hakuna njia mbadala ya kutatua tatizo la nyuklia la Korea Kaskazini ispoku njia za kidiplomasia na za kisiasa, kwa kuzingatia mazungumzo na pande zote zinazohusika. Tunatoa wito kwa wajumbe wa jumuiya ya kimataifa kuunga mkono mapendekezo yaliyotolewa na Urusi pamoja na China kupitia tamko la pamoja la Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi na China tarehe 4 Julai mwaka huu, Urusi imesema katika taarifa yake. "

Siku ya Alhamisi (Septemba 21) Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, alikosoa vikali kauli iliyotolewa na rais wa Marekani ambaye siku ya Jumanne iliyopita alitishia kusambaratisha Korea Kaskazini.

Wakati huo huo rais wa Korea Kusini Moon Jae-in,ambaye alitoa nasaha kwa Marekani akiitaka kutotumia nguvu za kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini. Lakini pia aliomba jumuiya ya kimataifa kuimarisha vikwazo, kama Pyongyang itaendelea na chokochoko zake.