MAREKANI-KOREA KASKAZINI-USALAMA

Marekani yafanya mazoezi ya kijeshi kwenye rasi ya Korea

Mazoezi ya kijeshi ya Marekani katika rasi ya Korea, Sptemba 23.
Mazoezi ya kijeshi ya Marekani katika rasi ya Korea, Sptemba 23. Steven SCHNEIDER / US ARMY / AFP

Marekani imefanya tena mazoezi ya kijeshi kwa pamoja na Korea Kusini, huku ndege zake mbili za kivita za kuangusha mabomu zikionekana kwenye anga ya rasi ya Korea.

Matangazo ya kibiashara

Ndege hizo zimefanya mazoezi ya kurusha makombora kutoka angani hadi ardhini katika maji ya bahari ya Korea Kusini.

Mazoezi hayo yanafanyika huku mvutano na uhasama ukiendelea kati ya Marekani na Korea Kaskazini, huku Korea Kaskazini ikiapa kuendeleza mpango wake wa nyuklia ukizidi.

Mazoezi hayo yalikuwa sehemu ya mpango mkubwa "wa kuzuia kupitia vitisho" vitendo vya Korea Kaskazini, jeshi hilo lilisema.

Ndege hizo za Marekani zilipaa kutoka kisiwa chake cha Guam katika Bahari ya Pacific siku ya Jumanne usiku kabla ya kuingia anga ya Korea Kaskazini na kufanya mazoezi katika Bahari ya Mashariki na Bahari ya Manjano, kwa mujibu wa jeshi la Korea Kusini.

Marekani imesema jeshi la wana anga la Japan pia limeshiriki mazoezi hayo.

Viongozi wa nchi hizi mbili wamekua wakitoleana maneno ya kashfa na kila mmoja kumshtumu mwengine kuhatarisha usalama wa dunia.

Donald Trump, katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, alisema kuwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un anaelekea "kujiangamiza".

Naye Kim Jong-un alimwita Trump kama mzee aliyepungukiwa na akili na kuahidi kumuweka sawa hivi karibuni.