Pata taarifa kuu
VIETNAM-TABIA NCHI-MAJANGA ASILI

Watu 37 waangamia kufuatia mafuriko Vietnam

Daraja liliharibiwa wakati wa mafuriko makubwa katika jimbo la Yen Bai, 11 Oktoba 11, 2 017 nchini Vietnam.
Daraja liliharibiwa wakati wa mafuriko makubwa katika jimbo la Yen Bai, 11 Oktoba 11, 2 017 nchini Vietnam. AFP
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Watu wasiopunga 37 wamepoteza maisha nchini Vietnam na 40 hawajulikani waliko kufuatia mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyotokana na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha kaskazini na sehemu za kati nchini humo, serikali imesema Alhamisi hii.

Matangazo ya kibiashara

"Jambo muhimu zaidi sasa ni kuunganisha nguvu zetu kwenda kutafuta watu wanaosadikiwa kutoweka, "Naibu Waziri Mkuu Trinh Dinh Dung amesema kwenye televisheni kutoka mkoa wa Hoa Binh kaskazini mwa nchi.

"Wakazi wanapaswa kuhamishwa kutoka maeneo yaliyo katika hatari," ameongeza mwakilishi huyo wa serikali ya Vietnam. Serikali ambayo itajiandaa vya kutosha kutokana na kuwasili katika siku chache zijazo na dhoruba ya kitropiki kutoka Ufilipino.

Mamia ya askari wanashirikikatika shughuli za uokoaji.

Mkoa wa Hoa Binh umeathirika zaidi na mvua zinazoendelea kunyesha tangu mwanzoni mwa wikii, huku watu 11 wakiripotiwa kupoteza maisha na wengine 21 walitoweka.

Watu wasiopungua 18 walipelekwa na maji usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi hii katika jimbo la Hoa Binh. Kumi na tano kati yao hawajulikano waliko.

Miongoni mwa waathirika katika jimbo la Yen Bai, mwandishi wa habari kutoka Shirika la Serikali la VNA, aliyepelekwa wakati mto uliofurika na kuharibu daraja siku ya Jumatano.

Nyumba barabara pia zimeharibiwa na mvua hizo.

Vietnam inakabiliwa na vimbunga zaidi ya kumi kila mwaka: kwa mujibu wa takwimu rasmi, karibu watu 170 wamekufa au kutoweka kutokana na hali mbaya ya hewa tangu mwanzoni wa mwaka.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.