Pata taarifa kuu
BANGLADESH-ROHINGYA-WAKIMBIZI-HAKI

Bangladesh kujenga kambi kubwa ya wakimbizi wa Rohingya

Wakimbizi wa sasa w Rohinya wataungana na wakimbizi wengine elfu 33 wa jamii ya Rohingya ambao wanaishi kwenye kambi za Kutupalong na Nayapara tangu miaka ya tisin
Wakimbizi wa sasa w Rohinya wataungana na wakimbizi wengine elfu 33 wa jamii ya Rohingya ambao wanaishi kwenye kambi za Kutupalong na Nayapara tangu miaka ya tisin REUTERS/Zohra Bensemra
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Serikali ya Bangladesh imetangaza kujenga kambi kubwa ya wakimbizi itakayowahifadhi wakimbizi wapatao laki nane wa jamii ya Waislamu wa Rohingya ambao wanavuka mpaka na kuingia nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Kambi hiyo itakuwa kubwa zaidi duniani na tayari imeibua mjadala ikiwa itaweza kuhudumia wakimbizi zaidi ya laki tano na nusu waliokimbilia Bangladesh tangu kuanza kwa oparesheni ya kijeshi Agosti 25 nchini Burma.

Wakimbizi hao wataungana na wakimbizi wengine elfu 33 wa jamii ya Rohingya ambao wanaishi kwenye kambi za Kutupalong na Nayapara tangu miaka ya tisini.

Shirika la Umoja wa Mataifa linayohudumia wakimbizi UNHCR linasema kufikia sasa dunia ina wakimbizi zaidi ya milioni sita nukta tano huku wengi wao wakiishi katika maeneo ya mijini yasiyopangwa.

Baadhi ya kambi kubwa zinazohifadhi wakimbizi duniani ni pamoja na Bidibidi nchini Uganda na Dadaab ya Kenya zenye wakimbizi zaidi ya laki mbili.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.