MAREKANI-KOREA KUSINI-KOREA KASKAZINI-USALAMA

Donald Trump azuru Korea Kusini

Rais wa Marekani Donald Trump (kushoto) na mwenzake wa Korea Kusini, Moon Jae-in, Novemba 7 Seoul.
Rais wa Marekani Donald Trump (kushoto) na mwenzake wa Korea Kusini, Moon Jae-in, Novemba 7 Seoul. REUTERS/Jonathan Ernst

Rais wa Marekani Donald Trump anazuru, Jumanne hii Novemba 7, Korea Kusini, hatua ya pili ya ziara yake barani Asia baada ya Japan. Kufuatia ziara hiyo maandamano mengi yanatazamia kufanyika katika miji mbalimbali nchini Korea Kusini.

Matangazo ya kibiashara

ais wa Marekani Donald Trump anashutumiwa kuchochea uhasama katika rasi ya Korea kwa kuzidisha vitisho vya mashambulizi nchini Korea Kaskazini.

Baadhi ya changanuzi wa masuala ya kivita wanaona kwamba uwezekano wa vita na Korea Kaskazini imekuwa sababu ya kwanza ya wasiwasi, amearifu mwandishi wa RFI mjini Seoul, Frédéric Ojardias.

"Katika shirika langu, wasiwasi kuhusu uwezekano wa vita umeendelea kungezeka tu tangu uchaguzi wa Trump mnamo mwezi Desemba. Kwa sasa hali imekuwa mbaya zaidi. Baada ya kipindi cha majira ya baridi, Marekani itakuwa imekamilisha maandalizi yake ya vita, na nadhani kuwa mgogoro halisi utaanza, "ameonya Woo Seung-hyeob, mmoja kati ya wanaharakati nchini Korea Kusini.

Lakini katika mji kama Seoul wenye wakazi milioni 25, ni vigumu katika vita au kunakotokea tetemeko la ardhi kuhamisha watu wote . "Wakati wa maafa, mahali pa usalama ni nyumbani: unapaswa kukaa nyumbani na kusubiri hali kurudi kuwa salama," ameongeza Bw. Seung-hyeob.

Rais Trump amemuelezea Rais wa Korea kusini Moon Jae-in kama mtu mwema na kusema kuwa watafanya kazi pamoja kuweza kushughulikia kitisho cha nyuklia kutoka Korea kaskazini.

Awali Rais Trump alielezea mbinu ya Rais Huyo wa Korea Kusini ambayo ni mbinu shirikishi dhidi ya Korea ya Kaskazini kama ya makubaliano na kwamba raia wa Korea Kusini walikuwa na wasiwasi na kauli za mabavu za Rais Trump kwamba zinaweza kuifanya Korea ya Kaskazini kuchukua hatua za kijeshi katika eneo hilo ya rasi.

Siku chache kabla ya kuwasili kwa Donald Trump nchini Korea Kusini, Rais Moon Jae-alihakikishia bunge lake kuwa hakuna hatua ya kijeshi upande wa Korea Kaskazini ambayo itawezekana bila idhni ya Korea Kusini. Lakini hiyo haitoshi kwa kuzuia wasiwasi wa maelfu ya waandamanaji wanaompinga Donald Trump wanaotarajiwa kumiminika katika mitaa ya Seoul.