MAREKANI-VIETNAM-USHIRIKIANO

Donald Trump azuru Vietnam

Hotuba ya Donald Trump katika Mkutano wa Apec, Danang, Novemba 10, 2017.
Hotuba ya Donald Trump katika Mkutano wa Apec, Danang, Novemba 10, 2017. REUTERS/Anthony Wallace/Pool

Baada ya Japan, Korea Kusini na China, Rais wa Marekani Donald Trump sasa anazuru Vietnam, hatua ya nne ya ziara yake barani Asia. Anashiriki katika jiji la Danang katika mkutano wa Apec, Jumuiya ya Ushirikiano wa Uchumi wa Asia-Pasifiki.

Matangazo ya kibiashara

Inatarajiwa kwamba atatoa maono yake kwa ukanda huo wakati wa hotuba yake, lakini tangu kufutilia mbali mkataba wa biashara wa TPP, ushirikiano wa Trans-Pacific, msimamo wa Marekani bado umezua maswali mengi .

Mwaka jana, ziara ya Barack Obama ilizua hali hali ya sintofahamu na msahnago mkubwa. Rais wa zamani wa Marekani alikuwa alivaa nguo za kawaida, huku akishikilia bia mkononi, katika mgahawa wa unaotembelewa na watu wenye mapato ya chini katika mji mkuu wa nchi hiyo. Hata hivyo, alitumia fursa ya ziara yake kuwatolea wito viongozi wa Vietinam kuheshimu zaidi haki za binadamu.

Mwaka mmoja baadaye, taswira hiyo imebadilika, Donald Trump baada ya kuchukua hatamu ya uongozi, suala la haki za binadamu halipewi kipaumbele. Kwa sasa anashiriki katika mkutano wa kilele wa uchumi wa Apec na inawezekana kuwa atakutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin wakati ili kujadili suala la Korea Kaskazini.

Hakuna anayetarajia maamuzi makubwa, lakini rais wa Marekani atatumia fursa ya mkutano huu ili kujaribu kuwahakikishia washirika wake, yeye ambaye wakati wa kampeni yake ya uchaguzi mwaka uliopita, alikua akisema "America First" ikimaanisha Marekani Kwanza, na hifo kusababisha hofu ya kufutwa kwa ahadi za Marekani kwa ukanda huo.